Header Ads

Uthibitisho Chid Benz Kukamatwa na Dawa za Kulevya, Upo Hapa!

Kuna taarifa zilitoka leo jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram
Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.

Imefahamika ni kweli msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea
uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo
ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.

Kwenye mahojiano na millardayo.com kamishna
msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika viwanja vya ndege
Tanzania amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii huyu alipohojiwa amekiri
kweli kuwa dawa hizo ni zake.

Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia
amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’

Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kusikiliza hapa

chanzo:millardayo.com

No comments

Powered by Blogger.