Header Ads

ALI KIBA AMMWAGIA SIFA DIAMOND KWA KUFANYA POA KATIKA JUKWAA LA FIESTA

Ni siku chache zimepita tangu tamasha la
Serengeti Fiesta lifanyike, ambapo tulishuhudia
baadhi ya wasanii wa hapa Bongo wakipata nafasi
ya kushare stage na wasanii wakubwa wa Afrika
kama Davido na Waje huku kutoka Marekani alikua
ni msanii T.I.
Ni ukweli usiofichika kua Fista ya mwaka huu
imekua gumzo kubwa hasa baada ya kutokea
mzozani kuhusu nani mkali zaidi kati ya Ali Kiba.
Japo kulikua hamna ushindani lakini mashabiki wa
wasanii hawa wawili wamekua katika marumbano
makali kuhusu alimfunika mwenzake.
Millard ayo kupitia Ayo Tv alipata nafasi ya kufanya
mahojiano na Ali Kiba kuhusu wasanii waliofanya
poa stejini na alikiba alianza kwa kusema ”
Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona kina Ommy
Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini
niliobahatika kuwaona wote wamefanya kazi nzuri,
nilimkuta Waje na Panto walifanya vizuri japo ni
nyimbo zao chache tunazijua ” akazidi kufunguka
zaidi kwa kuwataja wasanii ambao anaona yeye
walifanya vizuri ” Mr Blue amenifurahisha sana,
WEUSI wamefanya kazi nzuri…. kina Diamond
wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah ”
Habari imeandikwa na Eddie Sucre kwa msaada wa
Millard Ayo

No comments

Powered by Blogger.