ALGERIA YA KWANZA KUFUZU AFCON 2015, SENEGAL YAKALISHWA TUNISIA
TIMU ya taifa ya Algeria imefuzu Fainali za
Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco
kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
Malawi katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa
Mustapha Tchaker mjini Algiers usiku wa
jana.
Ushindi huo, unaifanya Algeria ifikishe pointi
12 baada ya kushinda mechi zote nne, wakati
Malawi inabaki na pointi zake tatu.
Mali, licha ya kufungwa 3-2 na Ethiopia katika
mchezo mwingine wa Kundi B jana, bado
wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi sita,
wakati Ethiopia ni ya tatu kwa pointi zao tatu
pia.
Mabao ya Algeria jana yalifungwa na Yacine
Brahimi, Riyad Mahrez na Islam Slimani.
Katika mchezo wa Kundi G, Tunisia ilipata
ushindi mwembamba wa nyumbani 1-0 dhidi
ya Senegal Uwanja wa Monastir mjini Tunis,
bao pekee la Ferjani Sassi dakika ya 94,
wakati Afrika Kusini imetoka sare ya 0-0 na
Kongo Brazaville mchezo wa Kundi A na
Burkina Faso imetoka 1-1 na Gabon.
Post a Comment