LORI LA MAFUTA LAANGUKA, LATEKETEA KWA MOTO - DAR
LORI la mafuta aina ya Scania likiwa
limesheheni dizeli likitokea bandarini jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta katika Barabara ya Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka kisha
kuwaka moto na kuteketea kabisa.
Wakati lori hilo likiwaka, mafuta yenye moto yalisambaa na kutaka kuunguza nyumba za jirani lakini Kikosi cha Uokoaji na Zima Moto cha Halmashauri ya Jiji, kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo limesababisha usumbufu
mkubwa kwa magari yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika
kwa shida.
HABARI/PICHA : GPL
Post a Comment