Header Ads

Dr Cheni afunguka Serikali isipokuwa makini, miaka 3 ijayo hakutakuwa na Filamu

Msanii mkongwe wa filamu nchini Dr Cheni amesema kuwa serikali isipokuwa makini baada ya miaka 2/3 kiwanda cha filamu za Tanzania kitapotea.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi TV hivi karibuni, Cheni alisema hata wauzaji wakubwa na
wasambazaji wameshaanza kupata hasara kutokana watu wanaotengeneza nakala feki.

“Unajua huko tunakokwendea kama hali hii itaendelea after four years hakutakuwa na movie ya
kitanzania inayouzwa,” alisema Cheni.

“Kwa sababu msambazaji ananunua master kwako labda amenunua milioni thelathini, ana mashine ya kurudufu, mpaka movie yako inatoka amepoteza
labda milioni 100, lengo lake arudishe kwanza
milioni mia halafu atafute faida kwa sababu analipa
kodi, analipia majengo.

Siku ya kwanza anaingiza movie sokoni leo, after
two days movies tayari ipo mikononi mwa watu
ambao ni wezi wa kazi.

Hata ile movie anayotegemea kuuza hatauza tena kwa sababu
watu tayari wanayo, Nani atafanya biashara namna hiyo? Ndio maana nakwambia serikali isipotilia
mkazo na movie ndio ina watu wengi sana wamejiajiri inakwenda kupoteza ajira hiyo.

Nataka nirudie tena serikali isipokuwa makini baada ya
miaka 2/3 game la movie halitakuwepo tena,”
alisisitiza Cheni.

Source; Bongo5.com

No comments

Powered by Blogger.