FAHAMU: LILE TUKIO LA MELI KUZAMA KOREA KUSINI LATENGENEZEWA FILAMU
LILE TUKIO LA MELI KUZAMA
KOREA KUSINI LATENGENEZEWA
FILAMU
WAANDAAJI wa tamasha kubwa la filamu
Korea Ya kusini BUSAN wametetea
uamuzi wao wa kuonesha filamu iliyoleta
utata nchini humo ya Driving Bell, 'The
Truth Shall Not Sink With Sewol'
Filamu hiyo inayoelezea maafa ya majini
yaliyo ikumba nchini hiyo imeonyeshwa
kwa mara ya kwanza siku ya mwisho ya
tamasha hilo kwa kuhudhuriwa na idadi
kubwa ya watu kuliko filamu zote.
Tamasha hilo ambalo lime hitimishwa
hapo jana ilionesha kwa mara ya kwanza
filamu hiyo fupi inayolezea kwa ujumla
jinsi uokoaji ulivyofanyika na kushuhudia
Wananchi wa korea kusini wakihangamia
katika ajali hiyo ya majini iliyotokea
nchini humo mwezi April mwaka huku
ikidaiwa kupoteza maisha ya watu zaidi
300.
Waandaji wanasema kuwa watu
wanahitaji kutoa maoni yao na sauti zao
zisikike, na kila filamu inayooneshwa
katika tamasha hilo ina umuhimu kwa
wananchini na wapo tayari kuwajibika
endapo lolote litatokea.
Muandaaji
Hapo awali ilitaarifiwa kuwa waaandaji
hao waliambiwa waiondoe filamu hiyo
kwenye orodha ya filamu
zitakazooneshwa ikiwa ni shinikizo
kutoka kwa baadhi ya wanasiasa
akiwemo meya wa jimbo la Busan.
Uamuzi wa kuonesha filamu hiyo fupi
umeiletea sifa waandaji wa filamu hiyo
baada kusifiwa na muandaaji wa filamu
fupi za Marekani Joshua Oppenheimer.
Post a Comment