SIMBA SC SASA MAMBO SHWARI...IVO MAPUNDA ARUDI KUOKOA LANGO
HOFU imeanza kupungua katika klabu ya
Simba SC kufuatia kipa namba moja wa
klabu hiyo, Ivo Philip Mapunda kuanza
mazoezi mjini Johannesburg nchini Afrika
kusini ambako klabu hiyo imewaka kambi
kujiwinda na mechi ya watani wa jadi dhidi
ya Yanga itayopigwa Oktoba 18 mwaka huu
uwanja wa TaifA, Dar es salaam.
Ivo aliyeumia kidole katika mazoezi ya
Simba zaidi ya wiki mbili zilizopita mjini
Zanzibar alioneka kuwa fiti, hivyo kuwatia
moyo wachezaji wenzake.
Joto lilizidi kupanda Msimbazi kufuatia
kipa aliyetegemewa kucheza mechi hiyo,
Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuumia ugoko na
katika mazoezi ya jana hakushiriki kabisa.
Kurejea kwa Ivo kutaliweka lango la Simba
katika mikono salama kwasababu Peter
Manyika asingeweza kuhimili presha ya
mechi hiyo.
Kabla ya kwenda Bondeni, Ivo aliuambia
mtandao huu kuwa Simba inazidi
kuiamarika na wana matumaini ya kufanya
vizuri mechi zijazo kuanzia ya Yanga.
“Mashabiki wasife moyo, tulianza kwa sare
tatu. Mengi yanazungumzwa, lakini hakuna
haja ya kushikana uchawi, kikubwa ni
kujiandaa na tunaamini tutaweza kufanya
vizuri”. Alisema Ivo.
Aidha, aliongeza kuwa kama Casillas
atasimama langoni haitakuwa na tatizo
kwasababu ni kipa mzuri, lakini atahitaji
kujiamini zaidi kwasababu hajawahi
kucheza kwenye mechi ya presha kama
hiyo.
Simba ipo kambini nchini Afrika kusini na
inatarajia kurejea siku moja kabla ya mechi
ya jumamosi.
Post a Comment