Header Ads

Nikki Wa Pili aamua kurudi chuo kusoma PHD baada ya kuona muda unapotea

Mwishoni mwa mwaka jana 2013 rapper Nikki Wa
Pili aliwahi kusema “Namuomba Mungu anipe PHD
nikiwa Kijana”, na hatimaye ndoto hizo zinaenda
kutimia.( Ingia hapa )
Nickson Simon anayefahamika kwa jina la kisanii
Nikki Wa Pili ambaye pia ni msemaji wa kundi la
Weusi, ameiambia BONGO 5 leo kuwa ameamua
kurudi chuo kwaajili ya kusoma PHD in
Development studies baada ya kuona ana muda
mwingi unaopotea.
“Kilichonisukuma ni kwamba yaani sasa hivi 100%
nafanya muziki, na navyokuwa nafanya muziki
hauandiki nyimbo kila saa hauendi studio kila saa,
unafanya muziki wakati una mood. Sasa kama
kijana nimeona natumia muda mwingi sana nakaa
gheto naangalia movie, nikaona huu muda naweza
nikafanya kitu kingine ambacho kwangu naona ni
productive(…) kwahivyo nikaona kukaa tu hivyo
muda unapotea bure unajua muda una thamani
sana”.
Nikki amesema tayari ameshaanza kufanya taratibu
za usajili na wiki ijayo ataanza kuingia darasani.
“Yaani hapa navyoongea na wewe naenda
kumalizia registration, masomo tutaanza wiki ijayo,
wiki hii tutaanza orientation UDSM.”
Rapper huyo wa ‘Sitaki Kazi’ ambaye mwaka jana
alihitimu shahada yake ya pili ya Uzamili katika
Maendeleo (Masters) chuo kikuu cha Dar es
salaam, ameelezea malengo yake atakapohitimu
PHD.
“Malengo yangu ni kwamba kuna hivi vitu vyangu
ambavyo navifanya binafsi nataka baadae vije viwe
vikubwa, kama hii taasisi yangu Twaonekana
nataka ije iwe kubwa, na pia nikienda shule
inaniongezea confidence, naweza kwenda
nikaongea na watu wengi wakaniamini. Nataka
kufanya biashara, na baadae sana kama nitafikiria
kufanya kazi labda nitahitaji kuwa mwalimu wa
chuo.”

Bongo5

No comments

Powered by Blogger.