PICHA : WAKAMATWA WAKILIMA SHAMBA HUKU WAKIWA UCHI - SIMIYU
ANGALIA PICHA ZA
WALIOKAMATWA WAKILIMA
SHAMBA HUKU WAKIWA UCHI
MKOANI SIMIYU
Bwana Makoye Kaboje, 42 akiwa na mkewe
Neema Kiwelu, 31 baada ya kunaswa.
Watu wanne wa familia moja, Makoye Kaboje, 42
(baba), Neema Kiwelu, 31 (mke) na watoto wao
wawili (majina yapo) walikutwa wakilima shamba
huku wakiwa watupu! Nyakati za saa 12 alfajiri
katika shamba la familia huku wakiwa uchi.
Tukio hilo la aina yake lilijiri alfajiri ya saa 12,
Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha
Bushingwana Kata ya Kalemila Wilaya ya Busega
mkoani Simiyu.
Tukio hilo ambalo mpaka sasa bado gumzo,
liliwashangaza wengi wakidai kuwa ni mara ya
kwanza kusikika katika mkoa huo mpya.Baadhi ya
wakazi wa kijiji hicho wanaamini si mara ya
kwanza kwa watuhumiwa hao kulima wakiwa
hawana nguo, bali siku ya tukio walichelewa hadi
jua linachomoza ndiyo maana walinaswa.
“Unajua wale wana kawaida ya kulima alfajiri ili
jua likitoka wanaacha kwa kuvaa nguo na
kuendelea kawaida. Sasa siku ile walijikuta
wamepitiwa mpaka jua linachomoza wao bado,
ndiyo maana walibambwa,” alisema mkazi mmoja
bila kutaja jina.
Uwazi lilipofanya mawasiliano na vyombo vya
ulinzi na usalama hususan jeshi la polisi,
lilikutana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Simiyu, ACP Venance Kimario ambapo alifungukia
kila kitu.
Msikie Kamanda Kimario: “Baada ya kukamatwa
wakilima watupu shambani, walifikishwa kituoni
kwa ajili ya mahojiano ambapo tulibaini kuwa,
wote walikuwa wa familia moja na walikuwa
wanaongozwa na baba yao.
“Walisema kulima bila nguo ni mbinu mpya
ambayo walipewa na ndugu yao mganga wa jadi
kwa kuwa kufanya hivyo kutaongeza mazao,
lakini hata hivyo, mganga huyo alifariki dunia
mwaka jana kwa maradhi.”
Kaimu Kamanda Kimario alisema watuhumiwa
wanashikiliwa katika Mahabusu ya Magu mkoani
Mwanza kwa madai ya kufanya ushirikina
hadharani.
source:UWAZI
Post a Comment