UN:'Kasi ya Ebola inatisha'
Idadi ya waliofariki kutokana na Ebola huenda
ikaongezeka katika miezi miwili ijayo
Afisaa mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na
janga la Ebola, anasema kuwa dunia inajikokota
katika vita vyake dhidi ya Ebola huku maelfu ya
watu wakiwa katika hatari ya kuambiukizwa
ugonjwa huo ifikapo Disemba mwakani.
Afisaa huyo Anthony Banbury ameambia baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kasi ya
maambukizi ya Ebola ni ya kutisha na kwamba,
huenda ikashindikana kudhibiti maambukizi.
Wakati huohuo, idadi ya watu waliofariki kutokana
na Ebola tangu janga hilo kuanza imefika 4,447 ,
wengi wakiwa katika kanda ya Afrika Magharibi.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani,
WHO.
Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bruce
Aylward, pia alisema huenda watu 10,000
wakaambukizwa ugonjwa huo kila wiki kwa kipindi
cha miezi miwili ikiwa juhuudi za kimataifa
haziongezwa kasi kupambana na ugonjwa huo.
Bofya hapa kusoma zaidi BBC
Post a Comment