Mbowe: Rais Kikwete ‘hasomeki’
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
akizungumza kwenye kikao cha Kamati Kuu ya
chama hicho kilichofanyika Dar es Salaam, jana.
Kushoto ni Katibu Mkuu, Dk Willibroad Slaa,
Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa
Mohamed (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu
(Zanzibar), Salum Mwalimu. Picha na Said Khamis
Dar es Salaam na Iringa. Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe amesema
Rais Jakaya Kikwete haeleweki kwa
sababu mambo mengi wanayokubaliana
naye anayafanya kinyume.
Akizungumza Dar es Salaam jana kabla
ya kuanza kwa kikao cha siku mbili cha
Kamati Kuu ya Chadema (CC), Mbowe
alisema Rais Kikwete si mtu wa kupanga
naye ‘dili,’ na kutolea mfano
makubaliano kati ya Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD) na Rais
kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Tulikutana na Rais Kikwete katika kikao
cha TCD na kukubaliana kuwa Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa ufanyike Februari
mwakani ili tubadili sheria kwanza na
kuboresha daftari la wapigakura.
“Cha ajabu kupitia kwa Waziri Mkuu,
Serikali inasema uchaguzi utafanyika
Desemba mwaka huu,” alisema Mbowe.
TCD inaundwa na vyama vya siasa
vyenye uwakilishi bungeni ambavyo ni
CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, UDP
na TLP, huku vyama visivyo na
uwakilishi bungeni vikiwakilishwa na
chama cha UPDP kinachoongozwa na
Fahm Dovutwa.
Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa na
ofisi ya Waziri Mkuu ambayo kisheria
ndiyo yenye jukumu la kusimamia
uchaguzi huo, fomu ya mgombea
uenyekiti wa kitongoji ina sehemu 12
ambazo mgombea anatakiwa kujaza,
ikiwamo nembo ya chama chake cha
siasa na nembo ya halmashauri aliyopo.
Wakati huohuo, wanachama tisa wa
Chadema Mkoa wa Njombe akiwamo
Diwani wa Kata ya Njombe Mjini, Aggrey
Mtambo wamekamatwa na polisi kwa
mahojiano ya saa nne baada ya kuingia
eneo la Kituo cha Polisi kwa ajili ya
kufanya usafi kwa kile walichoeleza
kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 15
ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere.
Tukio hilo lilitokea saa nne asubuhi jana
na viongozi hao wa Chadema
walishikiliwa hadi majira ya saa tisa
alasiri walipowekewa dhamana.
Chadema walifika zilipo ofisi za polisi
wilayani Njombe, kwa lengo la kufanya
usafi katika kituo hicho, baada ya
kufanya usafi katika Soko la Wakulima,
Soko Kuu na Stendi Kuu ya Mkoa.
Mtambo aliliambia gazeti hili muda
mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana
kwamba, walikamatwa na kuwekwa
ndani kwa kuwa walifanya usafi eneo la
polisi bila kibali.
“Kwa mujibu wa polisi, wametukamata
kwa kuwa tulienda kufanya usafi bila
kibali na gari la taka tuliloenda nalo ni
kama tulitaka kuteka kituo, , ” alisema
Mtambo.
MWANANCHI
Post a Comment