PICHA: HOUSEGIRL AMNYONGA MTOTO NA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI
NGALIA PICHA HOUSEGIRL
AMNYONGA MTOTO NA KUMTUPA
KWENYE DIMBWI LA MAJI
Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la
Ester (14) yupo matatani kwa madai ya
kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa
kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito
kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake
kwenye dimbwi la maji machafu,
Mama wa Mtoto akiwa hospital baada ya
kuzimia.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa
mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa
katika Zahanati ya Kellen kutokana na
mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku
ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku
mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania
kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo
alimkubalia na kumuagiza mboga.
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa
zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto
wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita
ambapo habari zilisambaa kwamba kuna
maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea
kwenye dimbwi la maji machafu
linalotumika kumwagilia bustani za mboga
maeneo hayo.
mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule
ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari
waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa
marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na
kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia
mauti.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili
Jumatano iliyopita akiwemo mama wa
marehemu, walisema kwa siku mbili hizo
alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana
kuwa na mambo
ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio
aliamka akiwa amenyolewa nywele upande
mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi
aliamka akiwa amenyolewa nywele upande
mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa
akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni
ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa
marehemu.
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio,
hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi
akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya
lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye
kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho
ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa
eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue
mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa
ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi,
Kibaha
Post a Comment