BREKING NEWS: WAKILI DAMAS NDUMBARO ‘ATUPWA JELA YA SOKA’ MIAKA SABA
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi
TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro
kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa
miaka saba na faini ya kiasi cha pesa.
Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa
na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita
baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia
tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu
hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom,
wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara,
na Azam Tv.
Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na
kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza
kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na
havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na
kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya
sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema
kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa
mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya
kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.
Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia
uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha
faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza
kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya
Ligi amekanwa ‘ hadharani’ na vilabu huku
vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale
ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari.
Klabu zimesema alizungumza kwa ‘ utashi’ wake
mwenyewe, na si wao walimtuma.
‘ Kilichomuhuku’ ni yeye kutaka kubadilisha
maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila
kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na
kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya
utendaji ni kosa la kinidhamu.
Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa
hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu
basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini
yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe.
chanzo:shaffihdauda.com
Post a Comment