Header Ads

WAZIRI NYARANDU ATOA SOMO KWA TANAPA


Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro
Nyarandu, alipokuwa akizungumza na
vyombo vya habari katika mkutano wake
uliofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Mbeya
HIFADHI za taifa Tanzania (TANAPA)
imetakiwa kuainisha maeneo yote yenye
vivutio vya utalii ambayo
yanawezekekana kuendelezwa na
kuyatangaza kwa wananchi wote ili kila
mwenye uwezo wa kuwekeza apewe
nafasi.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa
Maliasili na utalii, Lazaro Nyarandu,
alipokuwa akizungumza na vyombo vya
habari katika mkutano wake uliofanyika
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
katika mapumziko mafupi wakati
akielekea mkoani Njombe kumuwakilisha
Waziri Mkuu.
Nyarandu alisema Serikali inamikakati ya
kuhakikisha Watanzania ndiyo
wanapewa vipaumbele vya kuwekeza
katika sekta za utalii kwa kujenga
nyumba za kulala watalii, kujenga
makambi, kujenga na kuendeleza vivutio
pamoja na kutembeza watalii.
Alisema jambo hilo litasaidia kuinua
sekta ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na
kuwahamasisha watanzania kutembelea
hifadi mbali mbali na sio kusubiri
wageni kutoka nje ya nchi.
Alisema ili kuongeza kasi ya watalii
kuingia nchini kila mwananchi anapaswa
kujifunza kukarimu wageni hususani
wahudumu wa mahoteli ambao
wamekuwa wakiwahudumia wageni kila
wakati ili wawe na moyo wa kurudi tena.
Kwa upande wa ujangili na mauaji ya
Tembo Waziri Nyarandu alisema hivi
sasa kuna mafanikio makubwa kutoka na
kila Mwananchi kushiriki kulinda hifadhi
na kuzuia majangili kuua wanyama ovyo
kama ilivyokuwa awali.
Alisema hivi sasa kuna ongezeko kubwa
la Tembo tofauti na kipindi cha nyuma
baada ya serikali yake kuweka mikakati
kabambe ya kuwakabili wawindaji wote
ikiwa ni pamoja na kuwafungia leseni
wawindaji waliokuwa wakiwinda
kinyume cha sheria na kuhusika kwenye
mauaji ya Tembo.
Aliongeza kuwa hata mfumo wa
kukabiliana na ujenzi holela wa makazi
na mahoteli ndani ya hifadhi za
wanyama umechangia kuongezeka kwa
uzalishaji wa Tembo ambapo alisema
kwa takwimu za mwaka jana kuna
ongezeko la tembo zaidi ya 70,000.
Alisema hivi sasa Serikali haina idadi
kamili ya tembo walipo nchini katika
mbuga zote ambapo imeshaingia
makubaliano na nchi wahisani ili
kufanya sense ya Tembo na Faru ili
Serikali iwe na idadi halisi ya wanyama
hao nchini.
Alisema kazi hiyo imeshaanza kufanyika
ambapo Mwisho wa mwaka huu
wanatarajia kupata majibu ambayo
Serikali itawangazia wananchi wote ili
wajue idadi ya Tembo na Faru waliopo
katika kila hifadhi na mbuga za wanyama
nchini.
“ Hivi sasa kusema ukweli kabisa mimi
Waziri hata nikiulizwa swali leo kuwa
tuna tembo wangapi nchini sina majibu
kwa sababu hakuna mtu anayejua na
wala hatujawahi kuhesabu jambo
tunalitarajia kulifanya sasa” alisema
Waziri.
Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments

Powered by Blogger.