SUAREZ AKIRI ILIKUWA NGUMU KUKUBALI UKWELI WA KUMNG'ATA CHIELLINI
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez
amesema ilikuwa ngumu kukubaliana na ukweli
wa kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini
katika michuano ya Kombe la dunia nchini
Brazil. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay
ambaye alijiunga na Barcelona akitokea Liverpool
kwa kitita cha paundi milioni 75 alifungiwa miezi
minne kutokana na tukio hilo. Akihojiwa Suarez
amesema alikuwa akiona vigumu kukubali
alichokifanya kwani yeye ni binadamu kama
walivyo wengine. Nyota huyo mwenye umri wa
miaka 27 amesema likuwa hataki kumsikiliza
yeyote au kuongeza na yeyote kwasababu alikuwa
hataki kukubaliana na ukweli. Suarez alimuomba
radhi Chiellini Juni 30 zikiwa zimepita siku sita
toka afanye tukio baada ya Uruguay kushinda bao
1-0 dhidi ya Italia, msamaha ambao ulipokelewa
na beki huyo na kueleza matumaini yake kama
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lingeweza
kumpunguzia adhabu hiyo. Kabla kuomba radhi
Suarez alikanusha kwa kudai kuwa aliteleza
bahati mbaya na uso wake kumuangukia Chiellini
jambo ambalo lilikuwa kama vichekesho kwani
tukio hilo lote lilionekana katika picha za video.
Post a Comment