Header Ads

Mwisho wa CCM miaka 10


Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Joseph Butiku, amekionya chama chake kuwa
kama hakitaachana na mwenendo wake wa sasa,
uwezekano wa kuwapo miaka 10 ijayo ni mdogo.
Katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini
kwake jijini Dar es Salaam ambayo alizungumzia
mambo mbalimbali wiki iliyopita, Butiku alisema
chama hicho kimejiengua kwenye misingi yake kwa
kiwango kikubwa, huku vitendo vya rushwa
vikikumbatiwa katika kusaka uongozi wa nchi.
“Si lazima iwepo (CCM), lazima ibadilike. Irudi iwe
CCM. Isipobadilika haitakuwa CCM kwa sababu
ukiacha kusimamia misingi, itakuwapo hewa.
Upepo ukiisha kwenye mpira hata wa gari,
inasimama,” alisema na kuongeza:
“Wanachama tunaoijua CCM ilivyokuwa sivyo ilivyo
leo. Na sioni aibu kusema hivyo. Mimi ni mtu
mzima sasa, nimekulia ndani ya CCM. Naijua, najua
gharama ya kuwa mwanachama na kiongozi wa
CCM ni kujitoa kwa kiwango cha juu kabisa
kuwatumikia watu, sivyo ilivyo sasa.”
Alisema CCM ina katiba na miongozo mizuri, lakini
haiheshimiwi na kwamba watu wanadiriki kuvunja
robo tatu ya misingi ya chama bila kuchukuliwa
hatua na kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa
chama.

Soma zaidi bofya NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.