Header Ads

Maaskofu katoliki wajadili ushoga

Maaskofu katoliki wajadili ushoga
Mkutano wa maaskofu Vatican
Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa
maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya
kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa
kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye
mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti
wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko
Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja
wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye
jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa
mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa
msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya
kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya
vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja
wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio
makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo
mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na
kuuita ya kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki
wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu
mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa
Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya
utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa
mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.

Bofya hapa kusoma zaidi BBC

No comments

Powered by Blogger.