YANGA SC KUCHEZA NA WABABE WA KENYA JUMATANO, COUTINHO NA JAJA KWA MARA YA KWANZA TAIFA
Kikosi cha Yanga SC kilichoshinda mechi zote za kujipima nguvu Zanzibar |
KOCHA
Mbrazil, Marcio Maximo keshokutwa ataiongoza Yanga SC katika mchezo wa
nne wa kujipima nguvu tangu ajiunge nayo akirithi mikoba ya Mholanzi,
Hans van der Pluijm Julai.
Yanga
SC itacheza na Thika United ya Kenya Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam katika mchezo huo maalum kujiandaa na msimu mpya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, unaoanza Septemba 20, mwaka huu.
Lakini Yanga SC itaanza na mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu, Azam FC Septemba 13, Uwanja wa Taifa.
Kocha Maximo akiwa na Wasaidizi wake katika moja ya mechi za Zanzibar |
Katika
mechi tatu za awali ambazo Maximo ameiongoza Yanga SC, imeshinda zote
visiwani Zanzibar, 1-0 dhidi ya Chipukizi Uwanja wa Gombani, Pemba na
2-0 mara mbili dhidi ya Shangani na KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Wachezaji
wapya kutoka Brazil, walirejea Dar es Salaam na kumbukumbu nzuri ya
kuifungia mabao timu yao hiyo mpya kwenye michezo hiyo, mshambuliaji
Geilson Santana ‘Jaja’ akifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya
Chipukizi, wakati kiungo Andrey Coutinho akifunga bao moja kile mechi
katika 2-0 za Shangani na KMKM.
Ligi
Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi Azam
FC wakianza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam Septemba 20, mwaka huu, wakati Yanga SC waliomaliza nafasi ya
pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo.
Washindi
wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine,
Mbeya Septemba 20 na washindi wa nne, Simba SC wataanza na Coastal Union
ya Tanga Septemba 21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United
watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga,
Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na
Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi
mkoani Pwani.
SOURCE: BIN ZUBERY
Post a Comment