Home
>
Unlabelled
>
IRINGA MAANDAMANO YA CHADEMA YAPIGWA STOP, WARUHUSIWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA
IRINGA MAANDAMANO YA CHADEMA YAPIGWA STOP, WARUHUSIWA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA
Frank Nyalusi, Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini |
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Iringa Mjini jana
limeshindwa kufanya maandamano ya amani kama ilivyotangazwa kwa kile
kilichoelezwa na Mwenyekiti wake, Frank Nyalusi “tumepokea zuio kali
kutoka jeshi la Polisi.”
Akizungumza
Jana Nyalusi alisema walitoa taarifa kwa jeshi hilo siku mbili
zilizopita wakielezea nia yao ya kufanya maandamano hayo ikiwa ni kuitikia
wito uliotangazwa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe wa kufanya
maandamano ya amani yasio na ukomo yenye lengo la kushinikiza kusitishwa
kwa Bunge la Katiba.
Alisema
pamoja na jeshi hilo kuwazuia kufanya maandamano hayo, jana hiyo hiyo
waliruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara uliotarajiwa kufanyika mtaa
wenye machinga wengi maarufu kama magari mabovu, Kitanzini.
“Kwahiyo
tutakuwa na mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mimi mwenyewe na
viongozi wengine wa chama kuanzia saa 10 jioni, hivisasa tupo kwenye
kikao cha kamati tendaji kuweka maazimio kuhusu zuio la maandamano hayo
ya amani” alisema kwa njia ya simu.
Akieleza
kushangazwa na maamuzi ya Polisi ya kuzuia maandamano yao, Nyalusi
alisema maazimio yatakayofikiwa katika kikao hicho atayatangaza kwenye
mkutano huo.
Wakati
Chadema wakidai kudhibitiwa kufanya maandamano hayo, Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jeshi hilo halijapokea barua
yoyote kutoka katika chama hicho inayoonesha wameomba kufanya maandamano
hayo.
Akitoa
ufafanuzi huo kwa njia ya simu, Mungi alisema “nchi hii kama zilivyo
nchi nyingine inaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni.”
Alisema
watanzania bila kujali wanatoka kundi gani ni lazima wafanye mambo
wanayotaka kufanya kwa kuzingatia sheria vinginevyo mkono wa sheria
utawafukuzia.
Alisema
mji wa Iringa upo shwari na kwamba jeshi la Polisi limejipanga
kikamilifu kukabiliana na hali yoyote ile itakayoonekana inataka
kuhatarisha amani
Aliwataka
wakazi wa Iringa kuendelea na shughuli zao kama kawaida na pale
watakahisi au kusikia kuna mtu au kikundi chochote cha watu kinataka
kufanya jambo linaloweza kuhatarisha usalama wao na wa mali zao, watoe
ushirikiano kwa kutoa taarifa Polisi.
SOURCE: francis godwin blog
Post a Comment