Picha: Polisi Wafanikiwa Kukamata Watu Wawili Wakisafirisha Magunia 8 ya Bangi - ARUSHA
Afisa
wa Jeshi la Polisi kutoka kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya Mkoani
Arusha D/Cpl Kaleb akiwaonyesha waandishi wa habari (Hawapo pichani)
magunia ya madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa yanasafirishwa
kutoka eneo la Olkokola wilayani Arumeru kuelekea Mkoani Tanga.
....
Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata watu wawili wakiwa
wanasafirisha magunia manne ya madawa ya kulevya aina ya bangi yenye
uzito wa kilogramu 173.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas amesema kwamba,
watu hao walikamatwa juzi saa 5:00 usiku katika eneo la Nduruma jijini
hapa ambapo walikuwa wanasafirisha madawa hayo kwa kutumia gari aina ya
Toyota Corolla lenye namba za usajili T. 592 AAP.
Aliongeza
kwa kusema kwamba, mafanikio hayo yalipatikana kutokana na ushirikiano
mzuri kati ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa na wananchi ambao walitoa
taarifa juu ya tukio hilo. Alisema mara baada ya taarifa hiyo askari wa
kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya mkoani ambao waliokuwa doria usiku
huo waliweka mtego eneo la Nduruma na kufanikiwa kulisimamisha gari hilo
lililokuwa linatokea eneo la Olkokola wilayani Arumeru kuelekea Tanga.
‘’Mara
baada ya upekuzi walifanikiwa kuyaona magunia hayo ambayo yaliwekwa
katika sehemu mbili; gunia moja lilikuwa kwenye ‘’boot’’ na magunia
matatu yalikuwa kwenye ‘’Seat’’ ya katikati. Alisema Kamanda Sabas.
Akiwataja
watuhumiwa hao Kamanda Sabas alisema kuwa ni Laizer Melau (35) Mkazi wa
Olkokola wilayani Arumeru na Richard Fanuel (38) Mkazi wa Mianzini
Jijini hapa pia ni dereva wa gari hilo. Alisema mara baada ya mahojiano
watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na tukio hilo na watafikishwa
mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Kamanda
Sabas aliendelea kuwashukuru wananchi wa Arusha kutokana na ushirikiano
wao mkubwa katika utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuwaomba
waendelee kufanya hivyo na Jeshi hilo litaendelea kuzifanyia kazi hali
ambayo itasaidia kudumisha hali ya amani na utulivu.
Post a Comment