Header Ads

YONDANI: NGOJA NIKUTANE NA OKWI UONE UBORA WANGU



https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSwzg9RHOohpJj6jxz3cm3lAp2qxl_I-i3SYM-N-CUic8TIgHVj
Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, ametamba kuwa yeye ni bora na anataka kulithibitisha hilo atakapokutana na Emmanuel Okwi wa Simba katika mechi baina ya timu hizo, Oktoba 12, mwaka huu.

Yondani amesema hakuna ubishi yeye ndiye beki bora kwa hivi sasa, hivyo anaamini hakuna mshambuliaji yeyote atakayemsumbua ndani ya uwanja, akiwemo Okwi ambaye anazungumzwa zaidi katika kikosi cha Simba.
Beki huyo ambaye wiki mbili zilizopita alimdhibiti vizuri mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu katika mechi ya Ngao ya Jamii, amekuwa akishirikiana vizuri na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye idara ya ulinzi kwa miaka kadhaa tangu alipotua akitokea Simba.
“Nilianza na Kavumbagu aliyekuwa anatamba sana kuwa atatufunga, sasa hivi nguvu na akili zangu nazielekeza kwa Okwi ambaye naye anatamba kwamba atatufunga, ngoja tuone,” alisema Yondani.

No comments

Powered by Blogger.