Nick Cannon Amejibu Tuhuma Za Kuvunja Ndoa Ya Amber Rose Na Wiz Khalifa
Siku mbili baada ya Amber Rose kufuata taratibu za kisheria akidai talaka kwa mumewe Wiz Khalifa, Nick Cannon ameendelea kunyoshewa vidole kuwa chanzo cha yote na kudaiwa kuchepuka na mrembo huyo kwa kipindi kirefu.
Chanzo kimeiambia TMZ
kuwa Nick ambaye hivi sasa ni meneja wa Amber Rose amekanusha tuhuma
hizo na kudai kuwa hajawahi kuchepuka na Amber na hahusiki kivyovyote na
uamuzi wake.
Ameeleza kuwa alikuja
kufahamu Amber Rose alikuwa na matatizo ya kifamili kupitia mwanasheria
wake wiki iliyopita. Nick anasema baada ya kufahamu hivyo wawili hao
walianza kushare masimulizi ya kuacha na kuachana.
Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Wiz na Amber Rose, kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa michepuko.
Post a Comment