Header Ads

MLIPUKO WAUA 12 CHINA


Taswira kutoka eneo la Kiwanda cha Nanyang ulipotokea mlipuko.
TAKRIBANI watu 12 wamefariki dunia huku 33 wakijeruhiwa katika mlipuko uliotokea jana katika kiwanda cha kutengeneza fataki jijini Liling katika Mkoa wa Hunan nchini China.

Moshi ukiwa umetanda katika eneo la kiwanda hicho.
Mlipuko huo ulitokea katika Kiwanda cha Nanyang ambapo mamlaka husika haikusema chanzo chake.
Matukio ya kulipuka viwanda vya fataki nchini China yamezidi kuongezeka ambapo mwaka jana mlipuko mwingine ulitokea katika kiwanda kilichopo Guangxi na kuua watu 11 huku 17 wakijeruhiwa.
Februari mwaka jana gari lililokuwa limebeba mafataki nalo lililipuka barabarani katika Mkoa wa Henan na kuua watu watano na kuharibu sehemu ya barabara.

No comments

Powered by Blogger.