Header Ads

BEKI AWAANGUKIA MASHABIKI SIMBA, ASEMA ATA JIREKEBISHA SANA



Wakati kikosi cha Simba kikitarajia kushuka uwanjani kesho Jumamosi kupambana na Polisi Moro katika mechi ya Ligi Kuu Bara, beki wa kati wa timu hiyo, Hassan Isihaka amewaomba msamaha mashabiki wa timu hiyo kutokana na makosa aliyoyafanya uwanjani Jumapili iliyopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Isihaka alifanya makosa kadhaa likiwemo lile la kuunawa mpira nje kidogo ya eneo la 18 ambalo lilikuwa na faida kwa Coastal, kwani ilijipatia bao kupitia kwa Rama Salim na kufanya matokeo kuwa 2-2.
“Naomba wanisamehe kwa yote yaliotokea katika mechi hiyo na wasinielewe vibaya kwani sikukusudia kufanya hivyo ila hali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya wakati nikijaribu kuondoa mpira kwenye eneo hilo la hatari,” alisema Isihaka.
Isihaka ni kati ya mabeki wanaochipukia katika kikosi cha Simba na wanaonyesha mwendo wa kuja kuwa kati ya wale bora baadaye.

Hata hivyo atatakiwa kujituma ili kuendelea kuimarisha kiwango chake kwa kuwa soka linabadilika kila kukicha na ushindani unapanda.

No comments

Powered by Blogger.