Header Ads

BOT Yasisitiza Sarafu Mpya Kuanza Kutumika Oktoba Mosi


 Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT Bw. Emmanuel Boaz (kulia) akionyesha sarafu mpya ya shilingi mia tano ambayo itaanza kutumika Oktoba Mosi mwaka huu.


Benki Kuu ya Tanzania imesisitiza kuwa sarafu mpya ya shilingi mia tano itaanza kutumika Oktoba Mosi mwaka huu kama ilivyopangwa hapo awali, sambamba na pesa ya noti kwa ajili ya manunuzi yote yenye thamani ya shilingi mia tano.
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT Bw. Emmanuel Boaz, amesema hayo leo katika mahojiano na East Africa Radio, ambapo amewatoa hofu Watanzania juu ya hisia kuwa sarafu hiyo itakuwa na thamani ya chini tofauti na ilivyokuwa noti ya shilingi mia tano.

Amesema ni kwa sababu hiyo benki kuu imekuwa ikishindwa kuziondoa noti chakavu na badala yake noti hizo zimekuwa zikibaki mtaani na kuleta usumbufu kwa watumiaji.

Aidha, Boaz ameongeza kuwa ujio wa sarafu hiyo kutaipunguza serikali gharama za mara kwa mara za kuchapisha noti mpya, ambapo amewataka wananchi kujenga utamaduni wa matumizi na utunzaji bora ya pesa kwa kuziweka kwenye pochi na kuzuia zisiiguze vitu vya mafuta, maji maji na hata vumbi
Ametaja baadhi ya sababu za kuiondoa noti hiyo katika mzunguko kuwa ni kutokana na kuchakaa haraka kwa sababu ndiyo pesa inayotumika mara nyingi katika manunuzi ikilinganishwa na aina nyingine za noti.
SOURCE: EATV


No comments

Powered by Blogger.