MAHAKAMA HAKIMU MKAZI KISUTU YAWAACHIA WAFUASI WA CHADEMA
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru kwa
dhamana washitakiwa watatu wenye kesi namba173 ya mwaka 2014, kwa kosa
la kumsindikiza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Makao Mkuu ya
Polisi.
Washitakiwa
hao ni Ngaiza Kamugisha ambaye ni mfuasi wa chama hicho, Katibu wa
BAVICHA Temeke, Benito Mwapinga na Elisante Bagenyi ambae ni mfuasi wa
chama hicho, walifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa dhamana
kufuatia maombi yaliyopelekwa na wakili wao John Mallya.
Akisoma
mashitaka hayo, mbele ya Hakimu mkazi Frenk Moshi, Wakili wa serikali
Benard Kongola alidai kuwa mshitakiwa huyo namba moja mwenye miaka (28),
mkazi wa Vingunguti alikuwa anakabiliwa na kosa la kutoa lugha chafu na
kukiuka amri za jeshi hilo alipokuwa makao makuu.
Alisema
kufuatia maombi hayo, washitakiwa wengine wawili ambao walitenda kosa
hilo hilo nao waliachiwa juzi kwa dhamana ya sh. mil.5 kwa kila mmoja,
huku mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Kamugisha alirudishwa rumande na
kutolewa jana kwa dhamana ya kiasi hicho.
Alisema
kuwa, kosa hilo alilitenda mnamo Septemba 18 mwaka huu, majira ya saa
11 asubuhi, katika maeneo hayo ambapo lilitolewa onyo kuwa mtu asivuke
eneo hilo kutokana na taratibu za kiusalama.
Kwa
mujibu wa Kongola, Kamugisha alitumia lugha chafu kwa maafisa wa Jeshi
la polisi akiwemo Insipekta Zuhura, ambapo kauli hizo zingeweza
kusababisha uvunjifu wa amani.
Post a Comment