Header Ads

LAMPARD APIGA MBILI MAN CITY IKICHAPA SHEFFI 7-0, DOGO AVAMIA UWANJANI NA KUMFUATA

MANCHESTER City imesonga mbele katika Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup kufuatia kuichapa mabao 7-0 Sheffield Wednesday usiku huu Uwanja wa Etihad.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika ubao wa matokeo ukisomeka 0-0, lakini dakika ya pili tu ya kipindi cha pili, Frank Lampard akafungua karamu ya mabao. Lamprad alifunga mawili, dakika ya 47 na 90, sawa na Edin Dzeko aliyefunga dakika ya 53 na 77.




Mabao mengine ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England yalifungwa na Yaya Toure dakika ya 60 na kinda Angel Pozo dakika ya 88.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Caballero, Sagna, Demichelis, Mangala, Kolarov, Fernandinho/Boyata dk69, Navas, Toure/Pozo dk63, Lampard na Milner/Sinclair dk72, Dzeko.
Sheffield Wednesday: Kirkland, Buxton, Lees, Zayatte, Mattock, Coke/Dielna dk60, Maguire, Palmer/Helan dk69, Maghoma, May na Madine/Nuhiu dk60.
Lampard kulia akipongezwa na mchezaji mwenzake baada ya kuifungia Manchester City mabao mawili katika ushindi wa 7-0
 Shabiki mmoja wa Manchester City ameshindwa kujizuia baada ya kuvamia uwanjani wakati wa mechi ya Capital One kati ya timu hiyo dhidi ya Sheffield Wednesday.


Dogo huyo alishindwa kujizuia kuonyesha mapenzi yake kwa mkongwe Frank Lampard na kwenda moja kwa moja kupata naye selfie (kujipiga picha kwa kutumia simu).
Hata hivyo, baadaye Polisi walimdaka dogo huyo na kuondoka naye uwanjani hapo, hata hivyo alionekana kutojali kiivyo.

   

No comments

Powered by Blogger.