Header Ads

RONALDO NI MASHINE, ANGALIA REKODI ZAKE HIZI HAPA




Cristiano Ronaldo ameonyesha ni mchezaji wa aina yake, mwenye uwezo mkubwa na tofauti na wengi.
Jana amepiga hat trick nyingine ndani ya kipindi kifupi katika mechi mbili mfululizo wakati Real Madrid ilipoiangukia Elche kwa mabao 5-1.

Hiyo inaonyesha kweli yeye ni mkali na miguu yake ya kushoto na kulia, pia kichwa chake vyote ni mashine ya mabao.
Baadhi ya rekodi zake:
·       Mabao mengi kwa msimu kwenye michuano ya Ulaya-17
·       Mchezaji pekee kushinda kiatu cha dhahabu (mfungaji bora) kwenye ligi mbili kubwa za Ulaya (Premier League akiwa na Manchester United na La Liga akiwa na Real Madrid)
·       Mchezaji wa kwanza kufunga bao dhidi ya kila timu kwenye La Liga kwenye msimu mmoja.
·       Mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na Madrid kwa msimu mmoja, alipiga 60.
·       Alifunga hat trik saba, ambazo hazijawahi kufungwa na yeyote akiwa na Real Madrid.
·       Mchezaji aliyefanikiwa kufunga mabao 250 katika kipindi kifupi zaidi akiwa na Real Madrid ukilinganisha na wengine wote.
·       Mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na timu ya taifa ya Ureno, ameishapiga 50.


MWAKA                                   MECHI  MABAO
2002-2003     Sporting Lisbon       31      5
2003-2009     Man United             292    118
2009-              Real Madrid            254    264
2003-              Ureno                      114    50

No comments

Powered by Blogger.