Header Ads

MAN UNITED YATAKIWA KUTUMIA PAUNI MILIONI 100, KUSAJILI BEKI WA KATI NA KIUNGO MKABAJI - NEVILLE

BEKI wa zamani wa Manchester United, Phil Neville anaamini klabu hiyo inahitaji kutumia kiasi kingine cha Pauni Milioni 100 ili kuimarika kwa ushindani wa taji la Ligi Kuu ya England.Tyler Blackett (left) and Smalling were among those to struggle in the embarrassment at Leicester on Sunday
Timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, ilimuingiza sokoni kocha wake, Louis van Gaal kumwaga zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa manunuzi ya Angel di Maria, Luke Shaw, Ander Herrera, Marcos Rojo, Daley Blind na Radamel Falcao aliyechukuliwa kwa mkopo.
United iliyokwama kusajili beki wa kati, imejikuta kwenye tatizo la safu ya ulinzi msimu huu kutokana na Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans ama kutokuwa vizuri kimchezo au kutokuwa fiti, wakati kinda Tyler Blackett anaangushwa na uzoefu licha ya kupewa majukumu.


The Barclays Premier League table
Msimamo wa Ligi Kuu England hadi sasa
Na Neville anaamini hilo ni tatizo kubwa ambalo bado linahitaji ufumbuzi.
"Nafahamu United imetumia Pauni Milioni 150,"amesema.
"Nafikiri kuna uhamisho mwingine wa wachezaji wawili wa kiwango kile kile cha fedha unahitajika - labda Pauni Milioni 100- kabla hata hawajafikiria kushinda taji.
"Bado kuna nafasi muhimu katika timu zinahitaji kujazwa. Nafikiri nafasi ya beki ya kati wazi ni muhimu. Kiungo mkabaji au kiungo wa kati anahitajika kuongezwa pia. Hakukuwa na mabeki wa kati wa kiwango cha dunia sokoni usajili wa msimu huu. Nafikiri hiyo ndiyo sababu katika madirisha mawili yajayo ya usajili, United itapaswa kutafuta beki wa kiwango cha kidunia,"amesema.

The 28-year-old was appointed Manchester United captain at the start of the season by  Louis van Gaal
Michael Carrick (centre with Chris Smalling and Ryan Giggs) could play centre-half for Manchester United

HATA HIVYO MAN UNITED IMEONEKANA KUWA NI  'KISIWA CHA MATATIZO'...HILI NALO UGONJWA WA MOYO KWA VAN GAAL

BEKI Jonny Evans anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kuumia kifundo cha mguu Manchester United ikichapwa mabao 5-3 na Leicester City Jumapili.
Evans, ambaye ana historia ya maumivu ya enka na alihitaji upasuaji miaka miwili iliyopita, bado anataabika na tatizo hilo baada ya kuumia kipindi cha kwanza Uwanja wa King Power.
Beki huyo Ireland Kaskaini alifanyiwa vipimo Jumatatu na majibu ya awali yanaonyesha atakuwa nje kwa wiki nne.

Jonny Evans akisaidiwa kuondoka uwanjani baada ya kuumia enka dhidi ya Leicester

Huku Phil Jones akipona maumivu ya nyama na Tyler Blackett anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Leicester, kocha Louis van Gaal anaumiza kichwa juu ya safu yake ulinzi kuelekea mechi na West Ham Jumamosi Uwanja wa Old Trafford.

Jonny Evans is helped off the pitch after injuring his ankle at Leicester
The Norther Irish defender covers his face with his shirt as he trudges off
Marcos Rojo and Chris Smalling are due to line up together in central defence vs West Ham 
Marcos Rojo and Chris Smalling are due to line up together in central defence vs West Ham 
Van Gaal tayari amemuarifu beki wa kushoto wa England, Luke Shaw kuanza kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 27 kutoka Southampton, na Marcos Rojo anatarajiwa kushirikiana na Chris Smalling katika beki ya kati.

No comments

Powered by Blogger.