CHAMA CHA WANANCHI CUF CHA LAANI KUPIGWA KWA WANAHABARI MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na
wanahabari kulaani kitendo cha kupigwa waandishi. Jambo lingine
alilozungumzia ni kuhusu mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali za
mitaa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
wakati akilaani kupigwa kwa waandishi wa habari na askari polisi wakati
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
alipokuwa akihojiwa makao makuu ya jeshi hilo. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Habari na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (katikati),
akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Habari, Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Uchaguzi,
Shaweji Mketo, Yussuf Kaiza kutoka Idara ya Vijana na Pavu
Wanachama wa CUF wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali wakichukua tukio hilo.
…………………………………………….
Dotto Mwaibale
CHAMA cha
Wananchi (CUF), kimelaani kitendo cha baadhi ya polisi kuwapiga
wanahabari wakati Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alipokuwa akihojiwa na Polisi Makao
Makuu ya Jeshi hilo mapema wiki.
“CUF
inalaani kwa nguvu zote kitendo kilichofanywa na polisi cha
kuwashambulia wanahabari ni kitendo ambacho hakivumiliki tunaomba askari
wote waliohusika kuwashambulia wanahabri hao walikuwa kazini
wachukuliwe hatua” alisema Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim
Lipumba.
Katika hatua nyingine chama hicho kimetoa
malalamiko yake kuhusianana na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za
mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14, mwaka huu.
Kimesema hadi wiki iliyopita kilikuwa na taarifa kuwa uchaguzi huo
utafanyika
Februari mwakani baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukamilisha
taratibu zote zinazohusiana na daftari la kudumu la wapiga kura, ikiwemo
kuwaandikisha wananchi wote hadi ngazi ya vijiji navitongoji.
Akizungumza
na waandishi wa habari, kwenye makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam
leo, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa. Ibrahim Lipumba ,alisema hawana
taarifa sahihi ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Alifafanua
kuwa taarifa walizozipata kupitia vyombo vya habari kuwa iliyotolewa
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda siku chache zilizopita,kuwa uchaguzi huo
utafanyika Desemba 14, mwaka huu, ingawa walipokutana na Rais Kikwete
alisema uchaguzi huo utafanyika Februari mwakani.
Prof. Lipumba, alisema hatua hiyo ilikwenda kinyume na
makubaliano
waliyoafikiana na serikali katika Mkutano wa Vyama vya Siasa
ulioandaliwa na TAMISEMI Julai 14 mwaka huu mkoani Morogoro kujadili
Kanuni za Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Alisema
katika mkutano huo walikubaliana kuwa uchaguzi huo usimamiwe na NEC
kuanzia uratibu na uandikishaji wapiga kura hadi mwisho ikiwa ni
suluhisho la muda baada ya Katiba Mpya kuchelewa kukamilika na
kutotumika kwenye uchaguzi huo.
Pia alidai walipendekeza madiwani wajumuishwe kwenye uchaguzi waserikali za mitaa kama ilivyokuwa ikifanyika kabla ya mwaka 2000
kwa kuwa ndiye kiongozi wa juu katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
Post a Comment