EXCLUSIVE: PHIRI AWAANZISHA KWIZERA NA OKWI, MESSI, CHANONGO KUTOKEA PEMBENI...KIONGERA BENCHI!
TOFAUTI na wengi walivyotarajia, kocha mkuu wa
Simba sc, Mzambia, Patrick Phiri amefanya mabadiliko makubwa katika kikosi
chake kuelekea mchezo wa jioni hii, ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya
Coastal Union.
Mkenya Raphael Paul Kiongera ameanzia benchi,
wakati Mganda Emmanuel Okwi ameanza katika kikosi cha kwanza.
Phiri amewaanzisha Piere Kwizera na Emmanuel Okwi sehemu
ya washambuliaji wa kati, wakati Haruna Chanongo anashambulia kutoka winga ya
kulia na Ramadhani Singano ‘Messi’ anashambulia kutoka kushoto.
Mkongwe Shaaban Kisiga ‘Malone’ ameanza kama
kiungo mchezeshaji, wakati mfungaji bora wa msimu uliopita, Amissi Tambwe
ameanza kama kiungo wa ulinzi.
Langoni atasimama kipa mkongwe Ivo Mapunda, wakati
kulia anaanza Miraji Adam na kushoto anaanza Mohamed Hussein ‘Tshabalala.
Walinzi wa kati ni Hassan Isihaka na Joseph Owino.
Wachezaji wa akiba ni Hussen Sharif, Nassor
Masoud, Said Hamis, Joram Mgeveke, Amri Kiemba, Uhuru Seleman na Rapahel Paul
Kiongera.
Kikosi cha Simba hiki hapa:
Post a Comment