Header Ads

Obama Alia na Islamic State, Aapa Kuangamiza


Rais Obama ameahidi kuangamiza Wanamgambo wa Islamic State

Rais wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya kujificha .
Bw Obama amesema kushiriki kwa mataifa kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.
Pia amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowataja kuwa wanamgambo sugu wa al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema wanalenga kuishambulia Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.

 
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/625/amz/worldservice/live/assets/images/2014/09/23/140923125321_isis_raqqa_512x288_afp.jpg
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa wakifanya mauaji na utekaji nyara
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria ni dalili tosha kuwa vita hivi sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei hiyo.

SOURCE: BBC

No comments

Powered by Blogger.