FAHAMU: Mwanzilishi wa kampuni ya 'Apple', chanzo cha kuwazuia watoto wake kutumia iPad, iPhone na iPod
Bidhaa za kampuni ya Apple zina mashabiki na wateja wengi duniani, hii inathibitishwa na foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye vituo mbalimbali duniani kununua toleo jipya la iPhone6.
Tumesikia watu wakiachana ama familia zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya Apple. Mwaka jana familia moja nchini China iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo huo.
Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake kutumia
iPhones, iPods wala iPads nyumbani kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.
“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda mwingi nyumbani kwa boss wake huyo alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha usiku na familia yake kwenye meza kubwa jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au computer. Watoto hawakuonekana kuwa addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza Isaacson.
Post a Comment