PICHA: Serengeti Fiesta Yaweka Historia Mjini Songea
Maelfu ya mashabiki wa mji wa Songea jana ijumaa walikusanyika katika uwanja wa Majimaji mjini humo kushuhudia shoo kali ya kihistoria iliyoporomoshwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Kwa
mara ya kwanza katika historia, shoo ya Serengeti Fiesta iliingia
katika viunga vya mji wa songea na shoo kali zilizokonga vilivyo nyoyo
za mashabiki wa mji huo mara baada ya kufanya shoo nyingine kali kwa
mafanikio katika mji wa morogoro.
Kama
ilivyo utamaduni wake wadhamini wakuu wa shoo hiyo kampuni ya bia ya
Serengeti kwa kutumia kinywaji chake kikuu Serengeti Premium Lager
iliwapelekea mashabiki wa mji huo wasanii nyota wanaotamba kwa sasa
katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, wengi wao wakitumbuiza katika
mji huo kwa mara ya kwanza.
Godzilla,
TID, Linex, Mr. Blue, Madee, Stamina, Barnaba, Ney wa Mitego, Linah,
Recho, Mo Music na Baraka Da Prince ni baadhi ya wasanii waliokuwa
wakisubiriwa kwa hamu na wakazi Songea.
Mbali
na shoo hiyo, shughuli nyingine iliyofanyika ni Serengeti Super Nyota
diva na mshindi atapata nafasi ya kuja kushuhudia shoo ya mwisho
itakayofanyika jijini Dar es salaam mwezi ujao. Ilishangaza kuona vipaji
vya ajabu walivyonavyo vijana hao wa Songea.
Kadri
jioni ilivyokuwa ikikaribia ndivyo maelfu ya mashabiki walivyoendelea
kumiminika kwa kwa wingi kuja kushuhudia shoo hiyo, sehemu kubwa ya
tiketi kwa ajili ya kuingia kwenye tamasha hilo ziliendelea kununuliwa
mapema kwenye milango ya saa 9 jioni kabla ya shoo kuanza.
Idadi
ya watu waliokuja kushuhudia tamasha la burudani la Serengeti Fiesta
ilikuwa kubwa kiasi ambacho kiliwashangaza hadi waandaji wa tamasha hilo
lililofanyika kwa mara ya kwanza katika hitoria yake mkoani hapo.
Uanzishwaji
wa screen za LED kubwa badala ya zile za kawaida zilizokuwa zikitumika
hapo awali zilionekana kuvuta hisia za wakazi wa mji wa Songea ambao
wengi wao waliipongeza Primetime Promotions kwa kufanya maandalizi
mazuri.
Shoo
ilidumu kwa zaidi ya masaa nane. Godzilla, TID na Madee ni baadhi ya
wasanii waliokonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliojitokeza uwanjani
hapo kabla ya msanii Ney wa Mitego na Stamina kupanda jukwaani na wimbo
wao walioshirikiana kuimba uitwao “Huko kwenu vipi”.
“Napenda
kuwashukuru mashabiki wa mjini songea kwa kujitokeza kwa wingi katika
shoo hii….kiukweli ilinishangaza na nafurahi kuwa hawakutuangusha
ukichukulia kigezo kwamba shoo hiyo ilikuwa ikifanyika kwa mara ya
kwanza mjini hapa katika mtiririko wa shoo zake za mwaka huu za
Serengeti Fiesta”…alisema Rugambo Rodney – Meneja Chapa wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager.
Kwa
mwaka huu waandaaji wa tamasha hilo walichagua mikoa 18 ambayo shoo
hiyo itapita na hii ni idadi kubwa ya mikoa iliyochaguliwa katika
historia ya tamasha hilo, mikoa iliyoongozeka ni 3 katika ratiba za
tamasha hilo, nayo ni Bukoba, Kahama na Songea.
Baada
ya Songea, tamasha la Serengeti Fiesta 2014 litaelekea na shoo zake
katika mikoa ya Mtwara, Mbeya, Dodoma, Singida likiwa na kauli mbiu yake
“sambaza upendo” kabla ya kuhitimishwa rasmi jijini Dar tarehe 18
Oktoba ambapo wasanii wa nyumbani watapata nafasi ya kutumbuiza jukwaa
moja na msanii toka Marekani T.I ambaye kwasasa anatamba na kibao chake
“No mediocre”.
Post a Comment