Header Ads

BALE AMGONGA SHABIKI NA GARI LAKE, KISHA AKAONDOKA


 Gari la mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Gareth Bale limepanda kwenye mguu wa mmoja wa mashabiki wa timu hiyo.

Hata hivyo, Bale hakujua kama alimkanyaga shabiki huyo mwanamama ambaye alikuwa kati ya wale waliokuwa wakiwania kupata saini yake.
Baada ya kutoka uwanjani kwenye mazoezi, mashabiki walilizunguka gari lake. Naye alijitahidi kupiga nao picha na kuwasainia.
Lakini wakati anaondoka alimkanyaga mwanamama huyo bila ya kujua. Hata hivyo, mwanamama huyo hakuumia sana na amesema amemsamehe Bale kwa kuwa ni kati ya wanasoka wanaomvutia.


No comments

Powered by Blogger.