BRENDAN ROGERS AKIRI LIVERPOOL KUSHUKA KWA KUMKOSA LUIS SUAREZ
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akielekeza wachezaji wake katika mazoezi yaliyofanyika jana uwanja wa Melwood
BRENDAN
Rodgers amekiri kuwa Liverpool kwa kiasi fulani imevunjika baada ya
kuondoka kwa Luis Suarez majira ya kiangazi mwaka huu.
Bosi huyo wa Liverpool amesema ushindi katika mechi ya watani wa jadi wa Merseyside kesho dhidi ya Everton itakuwa mwanzo mpya wa ligi msimu huu.
Majogoo hao katika dirisha la majira ya
kiangazi mwaka huu walisajili wachezaji tisa na kumuuza Suarez kwenda
Barcelona, lakini wameshindwa kuonesha makali yao.
Liverpool wamepoteza mechi tatu kati ya
tano walizocheza za ligi kuu England na tatizo kubwa limetokana na uwezo
mdogo wa kujilinda, lakini Rodgers amekiri kuwa ubora wao wa msimu
ulipoita umepungua sana.
Liverpool wanamkosa mshambuliaji hatari
Luis Suarez (juu) ambaye aliuzwa Barcelona kwa dau la paundi milioni 75
majira ya kiangazi mwaka huu.
Post a Comment