LEO NI WIKI MAALUM YA WATANI ENGLAND, RATIBA ZIMA IPO HAPA!!!!
PAMOJA na kuwa wikiendi hii itakuwa na mechi
10 za Ligi Kuu england kama utachukua zote za leo, kesho na keshokutwa, mbili
kati ya hizo ndiyo gumzo zaidi.
Mechi mbili za watani ambazo zitapigwa wiki
hii, tena siku moja na ndiyo zitakuwa gumzo zaidi.
Liverpool itakapokuwa nyumbani dhidi ya
Everton wakati Arsenal watawakaribisha wapinzani wao wakubwa Tottenham. Kazi
hizi ziko katika miji ya London na Liverpool.
Unaweza kuangalia mechi yoyote utakayo,
lakini hizi mbili zinaweza kuwa zinabeba ujumbe mzito zaidi kwa maana ya soka,
nia ya ushindi na upinzani unaotokana na historia kwa kuwa kabla, timu hizo
zilikuwa ‘mwili mmoja’.
Liverpool Vs Everton
Tokea mwaka 1955 mechi
hiyo imekuwa maarufu kama “The Merseyside
derby”, ndiyo mechi maarufu zaidi ya watani ambayo ilianza kupigwa kwenye ligi
ya England tokea msimu wa 1962–63 hadi leo.
Kiutamaduni
inaaminika ndiyo mechi ya watani yenye urafiki na upendo zaidi. Siku ya mechi
watu wanakaa pamoja badala ya kila watu kuwa na upande wao.
Hii inatokana
kwamba, timu hizo zilikuwa pamoja Anfield, lakini zikatengana lakini bado kila
familia ya jiji la Liverpool ina watu wanaounga mkono Liverpool, wengine
Everton.
LEO:
Liverpool haiko
katika kumi bora, iko nafasi ya 11. Inahitaji kuanza kushinda kwani katika
mechi tano imepoteza tatu na kushinda mbili, si hali nzuri. Wao Everton pia
hawako poa, katika mechi tano wameshinda moja, sare mbili wamepoteza mbili,
hivyo kila mmoja atataka kuinukia kwa mwenzake.
Timu Mechi Shinda Sare Poteza
Liverpool 181
71 58 52
Everton 181 52 58 71
Mechi inayofuata (Ferbruari 7, 2015)
Arsenal Vs Tottenham
Kwa mara ya
kwanza, Arsenal na Tottenham zilikutana Novemba 19, 1887 katika mechi ya
kirafiki ambayo hata hivyo haikumalizika. Kiiza kiliingia ghafla dakika tano
kabla ya mechi kwisha Spurs wakiwa wanaongoza 2-1, mwamuzi akamaliza mchezo.
Mechi ya
kwanza ya mshindao wakati huo ligi hiyo ikijulikana kama daraja lwa kwanza
ilikuwa desemba 4, 1909 na Arsenal ikaibuka na ushindi wa bao 1-0.
Hata hivyo
utani au upinzani mkubwa rasmi ulianza mwaka 1913, baada ya Arsenal kuhamia
kwenye uwanja wake ambao baadaye ulijulikana kama Highbury. Arsenal ndiyo
imeonekana kutawala zaidi katika mechi walizokutana za michuano mbalimbali
kuanzia Premier League, Kombe la Ligi, Kombe la FA na mechi nyingi.
LEO:
Upinzani ni
mkali na ushindani utakuwa juu kwa kuwa katika mechi ngumu, Spurs
wameishapoteza mbili katika mechi tano, lazima watake kushinda na Arsenal walio
katika nafasi ya hawajapoteza, lakini katika mechi tano, wameshinda mbili na
sare tatu, si mwendo mzuri.
Timu Mechi Shinda Sare Poteza
Arsenal
160 67 43 50
Tottenham 160 50 43 67
Mechi inayofuata (Ferbruari 2, 2015)
Tottenham Vs Arsenal
Arsenal FC
MAFANIKIO Tottenham
4
Ushindi mfululizo
4
10
Mechi bila ya kupoteza 12
3
Mechi nyingi kila ushindi 3
14
Mechi bila kufungwa bao 9
LEO JUMAMOSI:September 27, 2014
Post a Comment