Header Ads

COASTAL UNION YAIPA USHAURI TFF, KUHUSU USHIRIKINA UWANJANI

Na Mwandishi Wetu, Mbeya


KLABU ya Coastal Union imelishauri Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhakikisha wanakuwa wakali kwenye kidhibiti vitendo vya kishirikina vinavyojitokeza kabla ya kuanza michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara kwani hali hiyo inadumaza maendeleo ya soka nchini.
Hali hiyo isipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa timu za Tanzania kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa wanayocheza nje za nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Albert Peter mara baada ya usiku wa jana saa saba usiku mashabiki ambao inasadikika ni wa timu ya Mbeya City kumwaga madawa kwenye kambi ya Coastal Union jambo ambalo sio zuri.
 Amesema iwekwe sheria kali kwa timu itakayobainika kufanya ili kutokomeza vitendo hivyo.

Licha ya hayo amesema kikosi cha timu hiyo kimejipanga vizuri ili kuweza kuhakikisha kinafanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.