AZAM TV IMEFUNGUA MIANYA YA NEEMA LIGI KUU, LAKINI…
Mkurugenzi wa Azam Media Limited, Abubakar Bakhresa kulia akipeana mikono na aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage (kushoto) wakati wa kusaini Mkataba wa kipindi cha Simba TV mwaka jana. Katikati ni Mwanasheria wa Azam, Shani Chrstoms.
HISTORIA ya udhamini katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaanzia mwaka 1996, ilipojitokeza kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Ligi Kuu ikawa inaitwa Safari Lager Premier League, hata hivyo TBL iliamua kuachana na michuano hiyo mwaka 2001, baada ya aliyekuwa Waziri anayehusika na michezo wakati huo, Profesa Juma Kapuya kuvunja kanuni kwa kuongeza timu za kushiriki hatua ya pili ya michuano hiyo, kutoka timu sita hadi nane.
Mwaka uliofuata, Ligi Kuu ikaangukia mikononi mwa kampuni ya simu ambayo ndiyo ilikuwa inaingia nchini wakati huo, Vodacom na udhamini wao umedumu tangu wakati huo, tena ukiboreshwa siku hadi siku.Bado fungu la Vodacom halikutosha kuondosha matatizo katika Ligi yetu, kulikuwa kuna malalamiko ya fedha zinazotolewa ni chache na wakati mwingine zinachelewa pia.
Ikawa rahisi Ligi yetu kutawaliwa na timu mbili kubwa- Simba na Yanga kwa sababu zenyewe wakati wowote, popote zinapocheza huvuna mapato mengi ya milangoni.
Timu ambazo ziko dhaifu kiuchumi hazikuweza hata kuunda timu nzuri, achilia mbali kuziandaa vizuri- hivyo ikawa ni ligi ya piga ua, ama bingwa Simba au Yanga SC.
Mtibwa Sugar ilikuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa Bara nje ya Simba na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 1999 tangu Coastal Union ya Tanga ilipofanya hivyo mwaka 1988.
Bofya hapa kwa habari kamaili
source: BIN ZUBEIRY
Post a Comment