STEVE NYERERE AAIBIKA UWANJANI
NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani.
Mrembo huyo akikatiza mbembezoni mwa uwanja.
Baadaye mwandishi wetu alimfuta Steve na kuzungumza naye kuhusu tukio
hilo ambapo alisema: “Wale kunizomea ni haki yao ila mimi na mwenzangu
tumeona kama wametushangilia.”Alipoulizwa uhusiano wake na demu huyo,Steve aligoma kujibu badala yake alikimbilia kwa mwandishi mwingine wa Global Publishers (Musa Mateja) na kuomba msaada. Mrembo huyo alipotakiwa kuzungumzia tukio hilola kuzomewa na sababu za yeye kuvaa vile, alijibu kwa mkato: “Kuzomea ni haki yao, mimi nawaona kama washamba tu.”
Post a Comment