POLISI YAINGILIA KATI MKUTANO WA CCM, NA KUWATAWANYA KWA NGUVU, SABABU HII HAPA!!
|
||
Cuf wakifurahia hatua ya Polisi |
Ofisa wa Upelelezi wa Ilala, Daivd Mnyambunga katikatia akijadiliana jambo na viongozi wa CCM akiwaambia kuwa inatakiwa waondoke |
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Ernest Charles akiwasihi wafuasi wake wa CCM kuondoka |
Polisi wakiwa wanajiandaa kwa kazi |
Hapo Cuf walianzisha muzikii wakitaka kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao za mkutano |
Abdul Kambaya
|
Huyu jamaa alianza kujiandaa kwa mapambano akikunja suruali |
Akasimamiwa kuhakikisha kuwa kazi inafanyika na ndipo alitii na kisha wanachama wa CCM kutimka |
Polisi waliendelea kuimarisha doria la nguvu |
CCM haooo wakapanga viti vyao na kuondoka |
Polisi wakaendeleza doria |
Wananchi wakishangaa |
Wanamama wa CUF wakaanza kujimwayamwaya na muziki wao |
Hao walikuwa wana CCM kabla ya kuondolewa |
Hawa niwa wafuasi Cuf wakifurahia baada ya kuona CCM wameondolewa. |
Ilikuwa ni patashika |
ASKARI Polisi wa kituo cha Buguruni leo walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliokuwa wakifanya mkutano katika eneo la Buguruni Chama.
Hatua hiyo ilitokana na wanachama hao kukusanyika bila ya kuwa na vibali stahiki vya kuwawezesha kufanya mkutano wao huo ambao uliingiliana na mkutano wa Chama cha Wananchi, CUF ambao nao walikuwa wakifanyia mkutano eneo hilohilo.
Kutokana na mkanganyiko huo ambao awali ulisababisha kukunjana mashati kwa wanachama wa vyama hivyo viwili kabla ya Polisi kuwasili na kutuliza vurugu hizo.
Ilichukua takribani saa tatu jeshi la Polisi likiongozwa na Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolis wa Ilala, David Mnyambuga wakijadiliana na viongozi wa upande wa CUF uliokuwa ukiongozwa na Mkuu wa Habari na Uenezi wa Taifa wa chama hicho, Abdul Kambaya wakati kwa upande wa CCM ukiongozwa na Katibu wake wa Wilaya ya Ilala Ernest Charles.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea magari mawili ya Cuf yaliwasili ambapo moja liliziba magari ya Polisi kwa mbele huku jingine likiwa limebeba spika za kuhutubia.
Lile lililokuwa limebeba spika liliwasha muziki wakati mazungumzo ya viongozi wa CUF, CCM pamoja na Polisi yakiwa yanaendelea hali amabyo ilizua tafrani kwa kuwa wananchi wa CUF walianza kucheza na hali ambayo ilipelekea CCM nao kuwasha muziki.
Hali hiyo ilipelekea tafrani kabla ya Polisi kuzuia taaharuki hiyo na wakaendelea tena na mazungumzo, baadae iliamliwa kuwa wote wasitishe mkutano huo na kuondoka.
Kambaya akizungumza na gazeti hili alisema kuwa wamepewa vibali vyote kuanzia ofisi ya Mtendaji wa kata ya Buguruni hadi Polisi na hawawezi kusitisha mkutano huo.
Katibu wa CCM Ilala, Charles alisikika akiwataka wanachama wake kukubaliana na hoja ya Polisi kuwataka kuondoka kwa kuwa hata CUF wameambiwa hivyo lakini wanachama hao walikataa kutii amri na hivyo katibu huyo alipanda gari lake na kuondoka.
Ilichukua takribani nusu saa kisha CUF waliwasha tena muziki uliowahamasisha wanachama wake kucheza na kisha Kambaya akaanza kuhutubia wanachana wake huku akilaani kitendo cha CCM kuingilia mkutano huo, wakati hayo yakiendelea wanachama wa CUF walianza kusogelea spika za muziki wa CCM ambao nao waliwasha tena muziki wao kwa sauti ya juu.
Kutokana na dalili hizo za kuvunjika kwa amani, Polisi waliamua kuvamia eneo la CCM na kuamrisha kuzimwa kwa muziki huo na kisha kuwatawanya wanachama hao kwa mabomu ya machozi sita yaliyopigwa hewani.
Hali hiyo ilipelekea taharuki kubwa katika eneo la Buguruni huku wananchi wakikimbia hovyo huku wale waliokuwa kwenye daladala wengine kulazimika kushuka.
Baada ya takribani dakika 30 za tafrani Polisi waliendelea kuulinda mkutano wa CUF ambapo Kambaya aliendelea na kampeni ya chama chake hicho iliyokuwa ikihamasisha suala zima la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Post a Comment