Header Ads

ARSENAL - HATUJALI UPINZANI WATANI WA JADI TOTTENHAM

Tim Sherwood, kulia, anadhani uzito wa mechi ya watani wa jadi wa London kaskazini umepungua 

NAHODHA na kocha wa zamani wa  Tottenham,Tim Sherwood amelaumu kupungua kwa uzito wa mechi ya watani wa jadi wa kaskazini mwa London, wakati huu Arsenal akijiandaa kuikaribisha Spurs uwanja wa Emirates.
Kocha huyo mwenye miaka 45 ambaye alishuhudia Arsenal ikilala mara mbili katika uwanja wa White Hart Lane akiwa kocha msimu uliopita, anaamini wachezaji wasasa hawatambui umuhimu wa mechi hizo kwa mashabiki wa timu zote mbili.
Katika kolamu yake kwenye gazeti la The Independent, Tim Sherwood aliandika: "Kwasasa haina maana kwa wachezaji? nadhani tamaduni zimebadilika. Unawaona wachezaji wa timu pinzani wanazungumza au kukumbatia wakati wakijandaa kuingia uwanjani".

No comments

Powered by Blogger.