MWALIMU AKUTWA AMEFUNGWA MINYORORO KWA MIEZI NANE KANISANI
Ndugu
wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35)
ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa
la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko
Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo
kwa miezi
nane mfululizo.
Kwa mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus,
ndugu yao huyo alichukuliwa na mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa
jina la Doreen kutoka Songea mkoani Ruvuma Januari, mwaka huu bila
kuwataarifu ndugu, jambo lililowafanya wamfuatilie na kugundua
alipelekwa kwenye kanisa hilo kwa madai ya kufanyiwa maombi.
Dada huyo alisema kuwa aliamua kumtafuta
ndugu yake hasa baada ya kupata taarifa kuwa aliko amekuwa akishinda
huku amefungwa mnyororo mguuni, hali inayomfanya ajisaidie na kula
papohapo.
“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,” alisema Piencia Focus.
Naye kaka wa Galus, aliyejitambulisha kwa jina la Peter alisema baada
ya kupata taarifa kwamba mdogo wake yupo kwenye kanisa hilo aliamua
kufika kwa ajili ya kumchukuwa kistaarabu lakini cha kushangaza
alijikuta akiangukia kwenye mikono ya waumini hao wakidai yeye ni gaidi
na wakamkwapulia fedha zake.“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,” alisema Piencia Focus.
Peter alisema alipoachiwa alikimbilia Kituo cha Polisi Wazo Hill ambapo alifungua jalada lenye Namba za Kumbukumbu WH/RB/6364/14 WIZI TOKA MAUNGONI.
Peter alisema alilazimika kuungana na dada yake kwa kushirikisha na
vyombo vya usalama ambapo walifika kanisani hapo kwa mara nyingine ili
kumkomboa ndugu yao na kuwatia mikononi waumini waliomwibia fedha zake.
Waandishi wetu waliokuwa karibu na eneo
hilo walizinyaka taarifa hizo na kufika kanisani hapo ambapo
waliwashuhudia ndugu hao wakiwa na polisi wakimchukuwa mmoja wa
watuhumiwa waliodaiwa kumshambulia Peter na kuondoka naye.
Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kitendo cha polisi hao kumwacha
Galus akiwa bado amefungwa kwenye nguzo na mnyororo kanisani hapo
wakidai watamfuata baada ya kumpeleka mtuhumiwa wa unyang’anyi kituoni,
jambo ambalo halikuwa la kweli kwani hawakufika kwa siku hiyo.Waandishi wetu walishuhudia timbwili la aina yake kanisani hapo kati ya waumini wa kanisa hilo na ndugu wa Galus waliorejea kwa lengo la kumchukuwa ndugu yao baada ya awali kumpeleka kituoni mtuhumiwa wa kumshambulia Peter.
Waandishi wetu walipoomba kuzungumza na uongozi wa kanisa hilo ilishindikana na kujikuta wakishambuliwa kwa maneno huku wakitakiwa kuondoka mara moja katika eneo la kanisa hilo.
SOURCE: GPL
Post a Comment