Header Ads

Chadema ‘yawaacha polisi kwenye mataa’


Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), ‘kimewaacha polisi kwenye mataa’ katika maeneo mbalimbali nchini baada ya kutojitokeza kwenye maandamano na kuwaacha askari wakiwa wamejipanga barabarani na maeneo nyeti wakiwasubiri, lakini mjini Bukoba chama hicho kilifanya maandamano.
Mjini Bukoba polisi waliojihami jana walionekana wakizunguka mitaa mbalimbali tayari kupambana na wafuasi wa Chadema, ambao waliwapiga chenga na kuandamana katika Kata ya Kibeta kwa umbali wa takribani kilometa mbili wakiwa na mabango (pichani kulia) bila polisi kuwabaini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Gilles Muroto alisema walikuwa wamejiandaa kupambana na wafuasi wa Chadema kwa kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku nchi nzima.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Wilaya ya Bukoba, Baraka Vedasto alisema wangeandamana kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba.
Jijini Dar es Salaam, wafuasi 12 wa Chadema walikamatwa katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya chama hicho kutaka kufanya maandamano kwa makundi kufika katika ofisi hiyo.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA!!!

No comments

Powered by Blogger.