UPEPO MKALI WAZUA BALAA JIJINI DAR ES SALAAM
Upepo
mkali uliotangazwa na Malka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) kuwa
utakuwa mkubwa na mawimbi bahari ya Hindi umeanza kuleta athari jijini
Dar es Salaam kwa miti kuanguka ambapo leo majira ya saa sita mti wa
Mnazi mali ya Masjidi Mwenyeheri uliopo kando kando ya barabara ya bibi
Titi katika mtaa wa Zanaki kukatika na kuangukia barabarani na
kusababisha magari kushindwa kupita kwa muda.
Father
Kidevu Blog ilishuhudia Askari Polisi waliokuwa wakipita na gari la
doria PT 1145 wakisaiduiana na wananchi kuufunga katika gari hilo na
kuusogeza pembeni ili kuruhusu magari kupita kama kawaida.
Baadhi
ya wananchi walihoji uharaka wa watu wa jiji katika kuondoa vitu kama
hivyo kwa haraka tofauti na wanavyoweza kukamata mama ntilie na wauza
mitumba mitaani au kukamata magari yaliyoegeshwa pasipo hitajika na
kusahau majukumu yao mengine kama hayo.
Upepo huo pia uliangusha uzio katika kiwanja cha kilichopo makutano ya mtaa wa Samora na Mkwepu Dar es Salaam.
Post a Comment