BAADA YA VIJINI.....SASA MAUAJI YA VIKONGWE YAHAMIA MJINI.....MMOJA AUWAWA MJINI KAHAMA.
PICHA HII HAISADIFU UHALISIA
WAKATI Serikali wilayani Kahama,ikiwa
katika mikakati ya kukomesha mauaji ya vikongwe kwa kuwatambua kwa kuwapigia
kura wauaji wa kukata mapanga,tayari janga hilo limeingia mjini baada y mtu
mmoja juzi kuuawa kwa kukatwa mapanga kilometa chache kutoka katikati ya Mji wa
Kahama.
Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Ilindi katika Halmashauri ya mji wa Kahama,baada ya wauaji hao kumuua kwa kumkata mapanga Elias Hungwi {52} mkazi wa Kata ya Zongomera ambapo watu hao wanaokadiriwa kuwa sita walivunja mlango wa nyumba yake kwa kutumia jina la Fatuma.
Kwa Mujibu wa Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo,Ally matisho watu hao baada ya kuingia ndani waliingia
chumba alichokuwa amelala Hungwi pekee yake baada ya mkewe,Yasinta Lugaranzura
kumuacha chumbani kwake alale na wageni
wa kike waliokuwa wamewatembelea.
Matisho amesema baada ya
kufika humo ndani walianza kuomba wapewe Shiringi Milioni Mbili wakidai Marehemu
Hungwi alizipata fedha hizo baada ya kuozesha binti yake miezi miwili iliyopita
baada ya kuzikosa walimuua kwa kumkata mapanga.
Hata hivyo Hungwi miezi
miwili iliyopita amemuozesha Mtoto wake wa Kike kwa kiasi cha Shilingi Laki
Sita lakini wauaji hao waliomba kupewa Shilingi Milioni Mbili ambazo hazikuwepo
kwenye familia hiyo.
Jeshi la Polisi kupitia
Kamanda wake wa Mkoa wa Shinyanga;Justus
Kamugisha linawashikilia watu watano wana familia hiyo,wakiwemo wageni
waliofika hapo na kulala chumba cha Marehemu huyo na mkewe hali iliyofanya
alale chumba kingine mpaka alipopatwa na mauti hayo.
Post a Comment