UKWELI KUHUSU:WALE MAKOMANDOO WA NEPAL WALIYOKAMATWA NA IDARA YA UHAMIAJI JIJINI DAR, WAONYESHA NYUMBA YA MNYARWANDA WALIYOKUWA WAKILINDA-UWANJA WA NDEGE DAR
Juu na chini ni picha za wanajeshi hao wakiwa nchini mwao
wakilitumikia jeshi la nchi yao kabla ya kutimka na kukamatwa Tanzania.
Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam Grace Hokororo akizungumza kuhusu suala hilo
Komandoo
Sidhee Bahadurkatuwal (kulia) kutoka Nepal akionesha nyumba ya Mrwanda
aliyokuwa akiilinda kupitia kampuni ya Ulinzi ya Advanced Security
karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es
Salaam, akiwa na makomandoo wenzake kutoka Nepal,
Baadhi ya makomandoo wa kijeshi kutoka Nepal wakiwa wamevalia sare ya Kampuni ya Ulinzi ya Advanced katika nyumba hiyo.
Maofisa
wa Uhamiaji wakimhoji mama wa kitanzania aliyeolewa na mnyarwanda ambao
nyumba yao ilikuwa ikilindwa na Komandoo kutoka Nepal
---
Idara ya uhamiaji Jijini Dar es Salaam imewakamata raia 12 wa kigeni
waliokuja nchi kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa Jeshi la
Nepal na 8 kutoka nchini India walioletwa nchini kinyume na sheria kwa
kile walichosema ni maisha magumu nchini kwao.
Raia hao wamekamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya ESCOT iliyoko huko Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika operesheni maalum iliyoendeshwa na Idara ya Uhamiaji Jijini baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao waliwatilia mashaka.

Miongoni mwa wanajeshi hao wa Nepal, yumo komando mmoja wa jeshi hilo
ambyeo amedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya masuala ya
ulinzi katika nchi za Afrika na hivyo walishukia Tanzania kama kituo
kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.
Afisa wa Uhamiaji wa jiji la Dar es Salaam, Grace Hokororo amesema kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita katika nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine kama Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali.

Aidha, Hokororo amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiletwa na mawakala
ambao wamekuwa wakiwatoa katika nchi zao kwa ahadi la kuwatafutia kazi
katika nchi hizi jambo ambalo amesema linatafsiriwa kama biashara ya
binadamu.Mawakala waliowaleta watu hao hadi sasa hawajapatikana.
Aidha Bi Gace amewataka Watanzania kuwafuchia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadaye huleta madhara makubwa kama vile ya uhalifu na uuzwaji wa dawa za kulevya.
Aidha Bi Gace amewataka Watanzania kuwafuchia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadaye huleta madhara makubwa kama vile ya uhalifu na uuzwaji wa dawa za kulevya.
Post a Comment