HISIA MBAYA KATIKA MAPENZI
Miongoni mwa vitu vinavyochangia kuharibu
uhusiano wa kimapenzi ni hisia. Wapenzi wengi wameachana kwa sababu si kwamba
walithibitisha ubaya wa wenzao ila walijijaza wenyewe hisia mbaya na kujikuta
wamepoteza thamani ya kupenda. Hebu angalia hisia nane hatari ili uzikimbie
mapema kabla hazijakuharibia penzi lako.
1.
NASALITIWA
Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra
kwamba mwenza wako anakusaliti ni jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani
wa kupenda. Matokeo yake utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama
mke/mume kwa sababu tu ya kuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.
2.
TUTAACHANA
Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya
“ipo siku tutaachana”. Wanafanya hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha
wa mapenzi yao. Kusema kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga
ufa wa mapenzi. Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu
mbadala ya kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama
mnagombana na mwenzako kila siku.
Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba
hawayawezi mapenzi. Hata kama hawajaambiwa chochote kuhusu kutowatosheleza
wenza wao faragha hukimbilia kujihukumu. Hujaambiwa kama umecheza chini ya
kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kama una lolote linalokufanya uwe na hofu
muulize mwenzio.
4.
NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini
wana kasoro fulani ndiyo maana hawafikii viwango vya kupendwa kama
wanavyovihitaji. “Yaani mimi ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini
ufupi wangu ndiyo tatizo.” Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi
wanapendwa ile mbaya. Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
5.
NITAMUUA
Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye
mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwa sababu yoyote. “Nikimfumania na
mwanaume mwingine nitamuua.” Mtu anayetawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka
katika mtego mbaya kisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anachojiapiza hata kwa
sababu ndogo. Usifikirie hivyo maishani mwako.
6. NIMEKOSEA
KUCHAGUA
Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi
wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwa kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka
mikakati ya kumuongoza mwezio kuliko kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea
kumchagua. “Ningejua kama yuko hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!
7.
HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu
au minne pamoja bila kupata mtoto hufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa.
“Mmm, mwaka wa nne umepita bila mtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.” Kwa nini
msizae?Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwaze hivyo? Jipe
moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wa mwaka mmoja?
8.
UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa
wanapendwa sana, hukimbilia kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm
unanidanganya.” Atasema hivyo licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na
kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba
unapendwa usihisi unadanganywa, utapoteza bahati yako.
SOURCE: MR CLEVER
SOURCE: MR CLEVER
Post a Comment