MZAZI AMUA MTOTO WAKE KISHA KUMZIKA KWENYE KIBANDA CHAKE CHA UGANGA -KATAVI
Mtoto mwenye
umri wa mwaka mmoja na miezi miwili , Regina Geofrey ameuawa kikatili
kwa kunyongwa na baba yake mzazi Geofrey Kilngwa ‘Simbaiwe” (27) kwa
kuwa alizaliwa akiwa ameatanguliza makalio yake .
Baba
wa binti huyo ambaye pia mganga wa kienyeji anayeishi kitongoji
cha Mwikang’ombe, kijijicha cha Katuma ,wilayani Mpanda alitenda unyama
huo kwa mdai kuwa mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio yake ni
mkosi na nuksi kubwa katika shughuli zake hizo za uganga wa kienyeji .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari akizungumza na waandishi
wa habari amedai kuwa mzazi huyo aliyetenda uhalifu huo Julai 20
mwaka huu ambapo alikamatwa na jeshi la Polisi Agosti 26, mwaka huu..
Inadaiwa siku
hiyo ya tukio mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake
huyo alimzika kwa siri katika kibanda chake anachofanyia shughuli
zake za uganga wa kienyeji .
Akisimulia
mkasa huo Kamanda Kidavashari alidai kuwa mtoto Regina alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi mmoja .
“Ndipo baba
mzazi wa binti huyo alipolazimika kuanza kumuuguza kwa
siri pasipo mama yake mzazi kufahamu kwani alimdanganya
kuwa mtoto wao huyo amepelekwa kutibiwa na babu yake huko mkoani
Mwanza “ alieleza Kidavashari .
Inadaiwa
kuwa kibanda ambacho mtuhumiwa alikuwa akifanyia shughuli zake za
uganga kilikuwa mbali na makazi yake hivyo ilikuwa rahisi kumficha
mtoto wake huyo kwa zaidi ya mwezi mzima akimtibu bila mama
mzazi wa mtoto huyo kufahamu .
Kwa
mujibu wa kamanda Kidavashari ,wakazi wa kitongoji cha
Mwikan’gombe wakiongozwa na Mwenyekiti wao walimtilia
shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi zilizozagaa eneo hilo kuwa mtoto
Regina alikuwa ameuawa na baba yake mzazi na kuzikwa kwa siri .
Inadaiwa
wakazi hao na mwenyekiti wao waliamua kufika nyumbani kwa
mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake Regina ambapo alipinga
vikali lakini alipopekuliwa katika kibandani kwake walibaini kuweko
kwa tuta dogo lililkuwa limechimbwa siku za karibuni .
Kidavashari aliongeza
kuwa wakazi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao waliamua kufukua tuta
hilo na kukuta kichwa cha mtoto huyo kisha wakaitaarifu polisi .
Mama
ya marehemu aitwae Maria Exavery (22) alidai kuwa hakuhusishwa wala
kupewa taarifa kwamba binti yake huyo amekufa “Mie nilikuwa nafahamu
kuwa Regina yuko kwa babu yake , Mwanza akitibiwa “ alieleza .
Nae
Regina Kaboni (40) mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na
mtuhumiwa anadai kuwa alishirikishwakatika maziko ya binti huyo
“hata
hivyo nilishtushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa
kumzika mwanae bila ya kumshirikisha mkewe , nilipomuuliza
mtuhumiwa alidai kuwa kwa mila ya kwao mtoto aliyezaliwa kwa
kutanguliza makalio yake mama mzazi wa mtoto ni mwiko kushirikishwa
katika maziko ya mtoto huyo ‘ anadai
Kwa
mujibu wa Kidavashari watu wanne wakiwemo wazazi wa
marehemu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ambapo
watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awa;li
kukamilika ..
Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni pamoja na Regina Kaboni na Msolwa Jacob (29) mkazi wa kitongoji cha Mwikanga’ombe .
SOURCE: MALUNDE BLOG
Post a Comment