Mitandao ya kijamii inachangia kuharibu mahusiano ya kimapenzi na kuvunja ndoa
Bila shaka kila mmoja anahamu ya kujua kwanini
nimeamua kuzungumzia mitandao ya kijamii, inawezekana wewe ni miongoni mwa
waliyoathiriwa na tatizo hili.
Mitandao inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda
na kila mmoja anashauku ya kujiunga na mtandao mpya hasa kwa wale wenye simu
zenye uwezo wa kufungua mitandao hiyo.
Wakati mwingine tunashauriwa kuwa na kiasi kwa kila
jambo, ili tusilemewe, wengi wamelemewa na hata kujisahau kwa kutumia mitandao
hiyo, kwa mambo yanayoichefua jamii na hata kuvunja maadili.
Mfano utamkuta mtu anakutumia picha ya mtu akiwa
utupu kwenye whatsapp, facebook, Instagram, twitter, tango, viber na mingine
bila kujali uhusiano wake kwako au umri wake na wako wakati mwingine sijui ni
kukosa adabu.
Lakini unajiuliza lengo la huyo mtu kukutumia picha
hiyo ni nini, na wengine wanakesha kwenye mitandao hiyo wakiwa wanachart na
watu wasiyowafahamu, na kuwatumia picha za mikao mbalimbali pamoja na ujumbe wa
sauti.
Mahusiano mengi sasa yamekuwa katika wakati mgumu
baada ya baadhi yao kujiingiza kwenye hiyo mitandao na kujiachia na watu
wasiywafahamu vema, na kupokea ujumbe wa aina mbalimbali.
Mwanamke mmoja alinisimulia mkasa uliyokuta baada ya
kuwa na maongezi na mchumba wake wakati wakiwa katika maongezi jamaa alikuwa
busy akichart na wanawake tofauti.
Mwanamke
yule alikereka sana na hali hiyo na kuamua kupokonya simu ile ili kujua
kulikono? Baada ya kupokonya alikutana na haya:
mpenzi wangu uko wapi?
nipo
kitandani nimepumzika nakuwaza wewe malaika wangu?
Lakini
unaniita malaika wakati hata hatujaonana? Unavyongea tu mimi hoi, natamani
ungekuwepo hapa!!!!!
Usijali
we nitumie usafiri nije nikupe mambo?
Utaniua mtoto wa watu…..jamani wewe….. haya
nipigie…. Aaa tuendelee kuchati baby.
Mwanamke wa pili sasa kesho jitahidi tuwe wote
baby.
Wala
usijali niko kwa ajili yako hata leo ungetaka ningekuja,,,, kwani bado uko
kazini? Ndiyo lakini bado kidogo nitatoka hapa….. ningekuwa sijachoka
ningekupitia tukapumzike wote…
Jamani
fanya hivyo basi mbona unanirusha roho sana wakati unajua navyokupenda.
Mme
wa mtu akichart na kimada jamani wewe mtoto mzuri uko wapi leo nataka
tukapumzike wote…
Leo
baba yuko ila kesho kila kitu kitakaa sawa wala usijali..lazima nijali inamaana
ujua huyu mwanamke wangu nimeshamchoka sasa wewe, hutaki kuziba pengo hili.
Nakuja
ila unakumbuka nilikwambia kodi yangu inaishia mwezi huu, na mtoto wa dada
anadaiwa ada, na uliniambia utaninunulia gallax 4 sasa nahamu nayo kweli..
Hayo
ni mambo madogo sana ingawa mke wangu anatumia simu ya tochi lazima
nikufurahishe ila kodi huyu bibie amechukua ATM yangu sasa kuitoa kazi
kwelikweli, ila si unajua mimi ni wako mpenzi….
Haya
my honey nakusubiria kwa hamu kwa kweli maana mashoga zangu watanitangaza lazima
mwaka huu nimeshawaambia wakanitangaze niko na mtu wa nguvu lakini jamani waume
za watu mnajua kuhonga.
Huu
ndiyo Ukweli wa mawasiliano yanayofanyika katika mitandao mingi ya kijamii watu
wengi akiwemo wewe unayesoma makala hii inawezekana ndiyo tabia yako.
Lakini
kumbuka hakuna kilichokuwa na mwanzo kikakosa kuwa na mwisho hizi ni nyakati za
mwisho wewe uko upande gani?
Unadhani
michepuko kwenye mitandao ni dili au upumbavu? Neno la Mungu linasema watu
wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Baki njia kuu kwa
kumpenda, kumweshimu, mkumjali huyo uliye naye katika mahusiano ya kimapenzi,
kumbuka maamuzi yako ya leo ndiyo matokeo yako ya kesho
Post a Comment